Afe kipa, afe beki lazima wapigwe

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
11 Jul 2020
Afe kipa, afe beki lazima wapigwe

Pamoja na tambo nyingi za mashabiki wa Simba kuelekea mchezo dhidi ya watani zao Yanga, hakika wanapaswa kuwa na akiba ya maneno kwani mchezo wowote unaozikutanisha timu hizo huwa hautabiriki

Nilimsikia msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, akihojiwa na chombo kimoja cha habari akitamba kuwa kwao mechi ya Jumapili hakutakuwa na habari ya kufungwa, kutakuwa na matokeo ya ushindi tu kwa timu yao

Ukiangalia takwimu, katika misimu mitatu iliyopita, Simba wamepata ushindi dhidi ya Yanga mara mbili tu na Yanga ikishinda mchezo mmoja dhidi yao

Msimu huu Yanga imevuna alama nyingi dhidi ya Simba kwenye ligi, wakishinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mwingine

Wachezaji wa Yanga wamedhihirisha kuwa hawahofii kabisa kucheza na Simba pengine kuliko mashabiki wa timu hiyo wanavyofikiria

Yanga inayokwenda kucheza na Simba ni tofauti kabisa na ile iliyofungwa na KMC, ikapata ushindi wa taabu dhidi ya Kagera Sugar katika michuano hii ya FA lakini pia ikatoka sare na Azam Fc katika mchezo ambao wengi wanaamini hawakustahili matokeo hayo

Yanga ya 'kariakoo dabi' ni nyingine kabisa, inakuwa na wachezaji 11 wanaofanya kazi ya wachezaji 22 uwanjani!

Ni Yanga ambayo anakabwa mtu na kivuli chake! Ni Yanga ambayo hutaweza kuwaona nyota wa Simba kama kina Chama ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika mechi nyingine

Wale viungo wa Yanga pale kati huwa wanakuwa kama vitoto vya mbwa ambavyo vimekutana na ziwa la mama yao baada ya kulikosa kwa muda mrefu!

Saikolojia ya wachezaji wa Yanga hubadlika kabisa pale wanapokutana na Simba, ujasiri unaongezeka na hutashangaa kuona mchezaji yeyote anayepangwa katika mchezo huo, anafanya vizuri

Utakuwa mchezo mzuri kwa mashabiki ku-enjoy kwani ushindani utakuwa mkubwa. Ni mchezo ambao ukanda wote wa Afrika Mashariki utatupia jicho

Wakati Simba wataingia uwanjani wakisaka taji la pili msimu huu, kwa Yanga huu ni mchezo muhimu sana kwao. Mchezo huu umeshikilia nafasi yao ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao. Hakika ni mchezo ambao hawatakubali wafungwe kirahisi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
59m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’