Niyonzima atakuwepo mechi dhidi ya Simba - Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Jul 2020
Niyonzima atakuwepo mechi dhidi ya Simba - Eymael

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema kiungo Haruna Niyonzima hatakuwa sehemu ya kikosi chake ambacho kesho Jumatano kitashuka kwenye uwanja wa Kaitaba kuumana na Kagera Sugar

Hata hivyo Eymael amesema kiungo huyo fundi atarejea kikosini kwenye mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, Julai 12 2020

Akizungumza na Wanahabari katika mazoezi jioni ya leo, Eymael alisema wanatarajia upinzani mkali kutoka kwa Kagera Sugar, akiwasifu vijana wa Meckie Mexime kuwa wanacheza soka la kitabuni

"Tuko tayari kwa mchezo, tumefanya maandalizi mazuri, mashabiki watafurahia burudani nzuri kwani tunacheza na moja ya timu bora zinazocheza soka safi," amesema

"Niyonzima hatuko nae hapa mazoezini ndio maana hamkumuona, hatakuwepo kesho lakini tutakuwa nae kwenye mchezo dhidi ya Simba," aliongeza Eymael

Winga Bernard Morrison leo alishiriki mazoezi hayo akitarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo wa kesho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’