Bodi ya Ligi Kuu imeurudisha nyuma kwa siku moja mchezo wa ligi kuu kati ya Kagera Sugar dhidi ya Yanga ambao awali ulipangwa kupigwa Alhamisi, Julai 09, sasa utapigwa keshokutwa Jumatano Julai 08 kwenye uwanja wa Kaitaba
Taarifa iliyotolewa na TPLB mapema leo, imebainisha kuwa mchezo huo umerudishwa nyuma ili kuipa Yanga nafasi ya kujiandaa na mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili Julai 12
Aidha muda wa mchezo huo umepangwa kupigwa saa tisa Alasiri
ADVERTISE HERE