Kituo kinachofuata ni Biashara United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jul 2020
Kituo kinachofuata ni Biashara United

Baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kuifunga Kagera Sugar mabao 2-1 hapo jana, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea Musoma mkoani Mara kuifuata Biashara United kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu

Mchezo dhidi ya Biashara United utapigwa siku ya Jumapili, kwenye uwanja wa Karume, Musoma

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema wanakwenda Mara huku wakifahamu watakabiliwa na mchezo wenye ushindani

Baada ya kukosa ubingwa ambao umechukuliwa na watani zao Simba kwa msimu wa tatu mfululizo, Yanga imejiwekea malengo ya kumaliza katika nafasi ya pili

Lakini inakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu vya Azam Fc na Namungo Fc

Yanga iko nafasi ya pili ikiwa na alama 60, nafasi ya tatu ikiwa mikononi mwa Azam Fc yenye alama 59

Namungo inashika nafasi ya nne ikiwa na alama 56

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’