GSM yafunguka ishu ya Morrison

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2020
GSM yafunguka ishu ya Morrison

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amepigilia msumari katika taarifa ya Yanga waliyotoa kuhusu mchezaji Bernard Morrison kuongeza mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria

Mhandisi Hersi ameeleza kushangazwa na kauli zilizotolewa na mchezaji huyo kwa kuwa yeye kama Mwakilishi wa GSM, alishiriki katika mchakato mzima wa kumuongeza mkataba

"Majadiliano ya mkataba mpya yalifanyika mbele ya macho yangu, GSM tukihusika kila hatua na baadae akasaini mkataba mpya mbele ya Mwanasheria wa klabu ya Yanga. Nenda kaangalie TFF au FIFA katika mfumo wa usajili utakuta Morrison ni mchezaji wa Yanga mpaka mwaka 2022," alisema Hersi katika mahojiano na Wasafi FM

"Tulipata taarifa za Morisson kuanza kusumbuliwa na baadhi ya watu huku wakimuahidi kumpa pesa zaidi ya sisi tulizosainiana kwenye mkataba mpya ambao unaisha 2022 na kuna kipindi alikuja pia akaomba avunje mkataba ili aendoke kwa maana amepata timu nje ila mimi kama mimi ninachoweza kusema ni kwamba Bernad Morisson ni mali ya Yanga"

"Nilipata nafasi ya kuongea na kocha kuhusu usumbufu anaofanya mchezaji huyu na akaniambia kuwa uwezekano wa kuleta winga mkali zaidi yake upo ila kama tutamuuza kwa maana sΓ sa bado ana mkataba hadi 2022," aliongeza

Inaelezwa Morrison ana kawaida ya kuwa msumbufu katika vilabu alivopita na hata Yanga ilimsajili akitokea nyumbani baada ya kuvunja mkataba na klabu ya DC Motema Pembe ya DR Congo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’