Uongozi wa klabu ya Yanga umempiga faini ya Tsh Mil 1.5 winga Mghana Bernard Morrison kwa kufanya mahojiano na chombo kimoja cha habari akiwa kambini
Kulingana na utaratibu ulioanzishwa na klabu hiyo, hakuna mchezaji ambaye anaruhusiwa kufanya mahojiano na chombo chochote cha habari bila ya ruhusa ya uongozi
Aidha, kulingana na taarifa iliyotolewa na Yanga mapema leo, klabu imewakumbusha wachezaji kuzingatia kanuni hiyo
Katika hatua nyingine, uongozi wa Yanga umesema Morrison bado mchezaji halali wa timu hiyo mpaka mwaka 2022
Taarifa ya Yanga imesema nyota huyo aliongezewa mkataba wa miaka miwili March 20 2020 baada ya kuridhishwa na kiwango chake
Mkataba wake wa awali ulipaswa kumalizika Julai 14 mwaka huu
Yanga imethibitisha kuwa mkataba mpya umesajiliwa TFF na FIFA hivyo kuvitaka vilabu vinavyomtaka vifuate utaratibu
Katika mahojiano aliyofanya na gazeti moja, Morrison alidai kuwa hajasaini mkataba mpya Yanga