Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amewaita mashabiki uwanja wa Taifa kushuhudia burudani kutoka kwa timu yao watakapokuwa wakipepetana na Azam Fc katika mchezo ambao utapigwa saa kumi kamili jioni
Eymael amesema vijana wake wako tayari, wamepania kuondoka na alama zote tatu katika mchezo huo
"Tumefanya maandalizi mazuri, vijana wangu wameonyesha utayari kuelekea mchezo wa kesho (leo). Mashabiki waje kwa wingi kushuhudia burudani. Huu ni mchezo wetu wa kwanza nyumbani tangu ligi iliporejea. Hatutawaangusha," alisema Eymael baada ya mazoezi ya mwisho ya mabingwa hao wa kihistoria
Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza, Eymael hatakuwa tayari kupoteza alama sita dhidi ya wauza Ice Cream hao
Ni mchezo ambao utakuwa na ushindani lakini ni alama tatu pekee ambazo zitawapa furaha mashabiki