Baada ya kupokea ushahidi kutoka kwa mshambuliaji Bernard Morrison, uongozi wa klabu ya Yanga umepeleka malalamiko rasmi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakitaka hatua zichukuliwe kwa timu iliyokuwa ikijaribu kumsajili mchezaji huyo wakati akiwa na mkataba na Yanga
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Wakili Simon Patrick amesema wanaamini TFF watachukua hatua stahiki kulingana na ushahidi waliowasilisha
Juzi Patrick alifanya kikao na Morrison ambapo pamoja na mambo mengine, walijadili kuhusu tuhuma alizozitoa hivi karibuni kuhusiana na klabu ya Simba ambayo ilijaribu kumshawishi kwa kumpa fedha ili ajiunge nayo
Aidha Simba inatuhumiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo bila ya kuwasiliana na Yanga ambayo mwezi March ilimuongezea mkataba wa miaka miwili