Morrison awaita mashabiki uwanja wa Uhuru Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jun 2020
Morrison awaita mashabiki uwanja wa Uhuru Jumapili

Winga wa Yanga Bernard Morrison amewaraka mashabiki kujitokeza uwanja wa Uhuru kuwashuhudia nyota wao kwa mara ya kwanza baada ya miezi miwili ya kukosa kuwaona dimbani kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona

Jumapili, Juni 07 Yanga itachuana na KMC katika mchezo wa kirafiki ambao utatumika kuzipima timu hizo kabla ya kuanza mikiki mikiki ya ligi

Morrison amesema amewakumbuka mashabiki wake hivyo siku hiyo angependa kuwaona majukwaani hasa ikizingatiwa Serikali imeruhusu mashabiki kuingia uwanjani ingawa ni kwa utaratibu maalum ili kujikinga na maambukizi ya corona

"Tumewakumbuka mashabiki wetu, tumejipanga kuwapa burudani nzuri kwenye mchezo wetu wa kwanza baada ya mapumziko ya corona. Tunawaita waje watuunge mkono kwenye mchezo huo wa kirafiki dhidi ya KMC, " alisema

Morrison amerejea kikosini baada ya kupona majeraha madogo aliyokuwa amepata

Yeye pamoja na beki kisiki Lamine Moro walishiriki kikamilifu mazoezi ya jana, nahodha Papy Tshishimbi akibaki kuwa mchezaji pekee ambaye ni majeruhi

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’