GSM kumwaga 'bonus' kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jun 2020
GSM kumwaga 'bonus' kombe la FA

Uongozi wa Yanga umeweka mkakati wa kuhakikisha ubingwa wa kombe la FA unaelekea Jangwani msimu huu

Yanga itacheza na Kagera Sugar katika mchezo wa robo fainali ambao utapigwa uwanja wa Taifa, Juni 28

Baada ya matumaini ya kutwaa ubingwa wa VPL kufifia, mkakati uliopo ni kushinda FA ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandishi Hersi Said ambaye tangu mwaka jana, kampuni yake imeweka utaratibu wa kutoa 'bonus' kwa wachezaji wa Yanga katika baadhi ya mechi wanazoshinda, amesema wamepanga kuendeleza utaratibu huo hasa kwa michuano ya kombe la FA ili kuhakikisha wanashinda taji hilo

"Ligi itakaporejea, utaratibu wa kutoa bonus kwa wachezaji tutaendelea nao lakini sasa tutaweka mkazo zaidi kwenye michezo mitatu ya kombe la FA iliyobaki," alisema Hersi

"Kuna fungu kubwa limeandaliwa kwa ajili ya bonus za wachezaji ili kuhakikisha wanashinda taji la FA"

Kama Yanga itaiondoa Kagera Sugar, hatua ya nusu fainali itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba dhidi ya Azam Fc

Mchezo wa fainali utapigwa Rukwa mwishoni mwa mwezi Julai dimba la Nelson Mandela

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’