Hersi afichua washambuliaji wanaokuja Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jun 2020
Hersi afichua washambuliaji wanaokuja Yanga

Yule mbabe kutoka GSM ambaye anasimamia michakato ya usajili iliyo chini ya kampuni hiyo, Mhandisi hersi Said, amedokeza kuwa Yanga itashusha washambuliaji kutoka nchi ambazo ubora wa ligi zao uko kwenye tano bora barani Afrika

Hersi ameiambia Sport Arena ya Wasafi FM kuwa nyota hao wote ni wafungaji bora katika ligi zao

Lakini pia, Hersi amedokeza kuhusu mwamba Heritier Makambo, akibainisha ni kweli ni miongoni mwa wachezaji ambao wako kwenye rada za mabingwa hao wa kihistoria ingawa kwa sasa wanafahamu ana mkataba na klabu ya Horoya AC

"Kuna washambuliaji wawili tunawafuatilia, wote hao ni wafungaji bora wa nchi wanazotoka na wanatoka katika ligi tano bora Afrika. Makambo ni mchezaji ambae yupo pia kwenye rada zetu lakini kwa sasa ana mkataba wa miaka mitatu na timu yake Horoya AC, ametumikia mwaka mmoja"

"Kuhusu mshambuliaji wa pembeni (winga), tutasajili winga mwenye uwezo mkubwa sana barani Afrika," alitamba Hersi

Hersi amesisitiza kuwa mkakati walioweka ni kuona Yanga inatwaa ubingwa wa ligi kuu msimu ujao na kuwa kama jambo hilo halitatokea basi ni wao GSM ambao watapaswa kulaumiwa

"Hatukupata ubingwa mwaka jana, hakuna wa kumlaumu lakini kama hatutachukua ubingwa mwakani basi mtulaumu sisi," aliongeza Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’