Nawaelewa mashabiki wanaponilaumu - Molinga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 May 2020
Nawaelewa mashabiki wanaponilaumu - Molinga

Mshambuali wa Yanga David Molinga amesema kama mchezaji, anawaelewa mashabiki wanaomtupia lawama pale anapokuwa hafanyi vizuri

Molinga alijiunga na Yanga usajili uliopita akitokea klabu ya Reinaissance, amefunga jumla ya mabao tisa, nane kwenye ligi na moja kombe la FA

Mshambuliaji huyo mwenye 'mwili jumba', amesema mashabiki hujinyima ili kuingia uwanjani kushangilia timu zao, inapotokea wao wachezaji hawafanyi vizuri wanastahili kutukanwa

"Mimi ni mchezaji wa kigeni, nalipwa mshahara mzuri, nakaa mahali pazuri, yaani napata kila kitu. Fikiria shabiki alikuwa na elfu moja tu ndani, akaitumia kuingia uwanjani kuishangilia timu yake, inapotokea simpi furaha huyu shabiki ni sawa akinitukana"

"Nilipojiunga na Yanga mwanzoni mashabiki walikuwa hawanikubali. Wengi walisema sina uwezo lakini baada ya kucheza mechi sita, wapo waliokubali uwezo wangu. Kama mchezaji siangalii nini mashabiki wanasema juu yangu, nina wajibu wa kutimiza majukumu yangu wakati wote," alisema Molinga

Aidha Mcongomani huyo amefichua wakati akijiunga na Yanga, mkononi alikuwa na ofa kutoka klabu ya AS Vita ya huko DR Congo

"Nilitaka kujiunga na AS Vita lakini Zahera (Mwinyi) alinishawishi nije Tanzania kujiunga na Yanga, kama sio Zahera pengine nisingekuwa hapa"

Molinga ni miongoni mwa wachezaji ambao hatma zao ziko mkononi mwa kocha Luc Eymael kwani mkataba wake na Yanga unamalizika mwezi August 2020

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’