Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema atatumia mechi zilizobaki kujiimarisha kwenye kikosi cha kocha Luc Eymael
Nchimbi maarufu kama 'Duma', amesema amefuata ipasavyo program ya mazoezi aliyoachiwa na kocha hivyo yuko tayari kuuwasha moto pale ligi itakaporejea
Akiwa mmoja wa nyota wa kutegemewa kwenye kikosi cha Yanga, Nchimbi amesema pamoja na wachezaji wengine, watahakikisha wanamaliza msimu kwa kishindo
"Binafsi nimekuwa nikifanya mazoezi kujiweka sawa, nimefuata program ya Mwalimu hivyo nimefurahi ligi kurejea na niko tayari kwa asilimia 100," alisema
Nchimbi ni mmoja wa wachezaji ambao wamejihakikishia namba kwenye kikosi cha Eymael akiwa na uhakika wa kuendelea kukipiga na mabingwa hao wa kihistoria licha ya ujio wa nyota kibao wanaotarajiwa kusajiliwa dirisha la usajili litakapofunguliwa
Β