Kilichombeba Niyonzima kwa Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 May 2020
Kilichombeba Niyonzima kwa Eymael

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ameweka bayana kuwa kiungo wa Rayon Sports Ally Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji ambao anatamani kuwa nao kwenye kikosi chake msimu ujao

Niyonzima amekuwa akitajwa sana kuelekea jangwani pale dirisha la usajili litakapofunguliwa

Nyota huyo hucheza pamoja na fundi Haruna Niyonzima katika timu ya Taifa, ni chaguo la kwanza katika nafasi ya kiungo mkabaji ambayo Eymael amependekeza aletewe mtu wa kumpa changamoto nahodha Papy Tshishimbi

Eymael ambaye bado anapambana kurejea nchini kutokana na changamoto ya usafiri wa anga huko Ubelgiji, amesema anahitaji kiungo anayeweza kumudu vyema majukumu yake hasa upande wa ulinzi

"Nahitaji kiungo ambaye atakaa katika nafasi yake na kutimiza vyema majukumu ya kulinda safu ya ulinzi. Tumeyaona makosa kadhaa kwenye safu yetu ya ulinzi lakini mengine hayasababishwi moja kwa moja na mabeki. Hivyo tutatumia vyema dirisha la usajili kutatua mapungufu yaliyopo," alisema Eymael

Pamoja na kumudu vyema nafasi ya kiungo mkabaji, Niyonzima anaweza kucheza nafasi ya beki wa kati namba nne na tano

Eymael amefichua kuwa anapendelea wachezaji wanaomudu nafasi zaidi ya moja uwanjani kwani hiyo inamsaidia wakati wa changamoto ya upungufu wa wachezaji kutokana na kadi, majeruhi au kuumwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’