Wakati wowote ndani ya wiki hii, klabu ya Yanga na bosi kutoka La Liga, Carraca Antonio watasaini mkataba unaofungua rasmi ukurasa wa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa Uwendeshaji Yanga
Msemaji na Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema baada ya mkataba huo kusainiwa, awamu ya kwanza ya mchakato huo itaanza
Nugaz amesema Yanga imejiridhisha kuwa imefanya uamuzi sahihi kuwachagua La Liga kuwaongoza kwenye mchakato huo kwani ni kampuni ambayo ina uzoefu na imevisaidia vilabu vingi
"Kwa kuzingatia hili, tulimchagua La Liga kuwa mshauri, tunaamini kwamba ana sifa zinazotufanya kufika mbali kwenye mabadiliko," alisema Nugaz.
Pia alitoa wito kwa mashabiki na wanachama kutoa ushirikiano uongozi ili ndoto za kuibadilisha Yanga zifanikiwe kwa urahisi.
"Vitu vingi vitaathiriwa tunapokwenda kwenye mabadiliko katika suala la usimamizi wa klabu, idara ya masoko na idara zingine pia.
"Wote tufanye kazi kwa kushirikiana Mwenyekiti wetu Dk Mshindo Msolla ili tufike katika nchi iliyoahidiwa kwa urahisi na kuruhusu michakato ianze mapema"