Dante apania kurejea kikosi cha kwanza Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2020
Dante apania kurejea kikosi cha kwanza Yanga

Beki wa Yanga Andrew Vicent 'Dante' amesema atatumia mechi zilizobaki kumshawishi kocha Luc Eymael kumjumuisha kwenye kikosi chake cha kwanza

Tangu arejeshwe kikosini baadhi ya changamoto yake ya madai kumalizwa na GSM, Dante amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi mbelel ya Lamine Moro, Kelvin Yondani, Ally Mtoni na Said Juma Makapu

Hata hivyo beki huyo aliyetua Yanga akitokea klabu ya Mtibwa Sugar mwaka 2015, amesema anaamini ligi itakaporuhusiwa kurejea, atakuwa na nafasi ya kurejea kikosini

"Unajua muda kama huu kila mtu hafanyi mazoezi ya timu, tukienda tunaenda kuanza wote kwa pamoja ndio maana nakuambia tunaenda kuanza upya"

"Nitatumia nafasi hii vizuri kurejea katika kikosi cha kwanza, naamini kiwango changu kwamba suala la kucheza ni la muda na ndio maana siku zote siachi kufanya mazoezi, nitafanya mazoezi mchangani na nitacheza mpira," alisema

Pamoja na kutoonekana uwanjani kwa muda mrefu, mashabiki wengi wa Yanga bado wameonyesha kuwa na imani na beki huyo kisiki ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanaosubiri mikatana mipya Yanga

Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’