Nadir amtaja Zahera kuondoka kwake Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2020
Nadir amtaja Zahera kuondoka kwake Yanga

Nahodha wa zamani wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye baada ya kustaafu alikuwa Meneja wa timu hiyo, ametaja sababu iliyomfanya aache majukumu yake katika klabu hiyo aliyoitumikia kwa heshima kubwa

Nadir ambaye anashikilia rekodi ya kucheza muda mrefu pamoja na kunyanyua mataji mengi akiwa na Yanga, amesema hakuwa akikubaliana na utaratibu uliokuwa ukitumiwa na aliyekuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera

Mkongwe huyo kutoka visiwani Zanzibar amefichua kuwa hakuwa akifurahishwa na tabia ya Mcomani huyo ambaye alikuwa akianiaka masuala mengi ya Yanga kwa Wanahabari

"Mimi nilijiondoa mwenyewe ndani ya Yanga, sikufukuzwa. Kama Meneja wa timu baada ya kuona tunatofautiana sana na aliyekuwa kocha mkuu kipindi kile Mwinyi Zahera kwa kuwa alikuwa akiweka sana wazi mambo ya timu kwa waandishi wa habari," alisema

"Baadhi ya masuala yanapaswa kujadiliwa na viongozi na kuyapatia ufumbuzi ndani na sio kwenda kuyatangaza kwa waandishi wa habari"

Nadir kwa sasa ni Meneja wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' akiwa sehemu ya kikosi kilichofuzu fainali ya michuano ya CHAN kwa wachezaji wanaocheza ndani

Fainali hizo ambazo zilipaswa kufanyika nchini Cameroon, zinasubiri kumalizika kwa changamoto ya ugonjwa wa corona

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
8h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’