Eymael adokeza nyota wenye uhakika Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 May 2020
Eymael adokeza nyota wenye uhakika Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga LUc Eymael ametaja kikosi cha nyota ambao ataendelea kuwa nao msimu ujao huku akisubiri kuletewa nyota wapya aliowapendekeza

Eymael amewataja Ditram Nchimbi na Morrison kuwa wachezaji muhimu sana katika mipango yake ya msimu ujao, wengine wakiwa ni makipa Farouk Shikalo na Metacha Mnata na mabeki Lamine Moro, Kelvin Yondani.

Viungo ni Said Juma Makapu, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Papy Tshishimbi, Haruna Niyonzima na Mohammed Issa ‘Mo Banka’, huku kukiwa na maingizo mapya katika nafasi za mabeki wa pembeni na mawinga kutegemea na hali ya kiuchumi Jangwani itakavyoruhusu.

Lakini kama mambo yakienda ndivyo sivyo, mabeki wa pembeni watabaki wale wale, yaani Juma Abdul (kulia) na Japhary Mohammed (kushoto), huku mawinga wakiwa ni Mapinduzi Balama na Patrick Sibomana.

Hata hivyo, kati yao, iwapo mambo yatakwenda kama yalivyopangwa kwa Wanajangwani hao kufanikiwa kusajili wachezaji wote waliopendekezwa, wapo watakaounda kikosi cha pili.

"Kama bajeti itaruhusu, nataka kuwa na vikosi viliwili vya nguvu ambavyo chochote kinaweza kucheza na kupata ushindi. Lengo letu ni lile lile kuwa msimu ujao Yanga iwe bingwa wa Tanzania," Eymael amenukuliwa na gazeti la Bingwa

"Nimekuta wachezaji wengi na wenye uwezo ndani ya timu, lakini kilichokuwa kinatukwamisha, baadhi yao hawakuwa na mazoezi ya kutosha na wengine kuwa na majeraha ya muda mrefu, ndio maana tumeshindwa kutoa upinzani katika ligi.

"Unakuta mchezaji ni mzuri na mashabiki wanamuamini sana, lakini ukimpanga tu, anatoka na majeraha, hii inamaanisha kuna ambao wanatakiwa kufanyiwa tiba kabla ya kuanza msimu," alisema.

"Kwa wachezaji niliowapendekeza, iwapo watasajiliwa wote, hakuna timu itakayotuzuia kutwaa ubingwa msimu ujao."

Eymael amesema atarejea nchini wakati wowote baada ya Serikali ya Ubelgiji kuruhusu safari za kutoka nje ya nchi hiyo kutegemea na maendeleo ya janga la virus vya corona.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
12h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
17h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
21h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’