Mtibwa Sugar yamkomalia Humud

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 May 2020
Mtibwa Sugar yamkomalia Humud

Licha ya kuhusishwa sana na Yanga, uongozi wa Mtibwa Sugar umesema hauna mpango wa kumuacha kiungo wao mkabaji Abdulhalim Humud

Msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema Humud bado ana mkataba na wakatamiwa hao na hawafikirii kumruhusu akajiunge na Yanga au timu nyingine yoyote hapa nchini

"Humud ni mchezaji wetu muhimu, hatufikirii kumuacha akajiunge na timu yoyote hapa nchini labda apate nafasi nje ya nchi," amesema Kifaru

"Tumemfanya Humud awe bora, ni mchezaji tunayemuhitaji sana katika malengo yetu ya msimu ujao hivyo ataendelea kubaki Manungu," aliongeza Kifaru

Kifaru amesema Humud ni mfano wa kazi ambayo Mtibwa Sugar wamekuwa wakiifanya kwa miaka mingi kuimarisha viwango vya wachezaji pamoja na kuibua wachezaji wapya

"Tunajivunia kuwa na rekodi ya kutoa wachezaji wengi ambao wanatamba hapa Tanzania. Mfumo wetu wa kukuza vipaji kuanzia U17 na U20 umekuwa na manufaa makubwa"

"Unaweza kusema Mtibwa Sugar ndio chuo kikuu cha kutengeneza vipaji vya wanasoka hapa nchini," alitamba Kifaru

Mtibwa Sugar ndio mabingwa wa ligi ya soka ya vijana wakiwa na timu imara za U17 na U20

Katika kikosi chao kinachoshiriki ligi kuu wanatumia wachezaji wengi wanaopita kwenye akademi yao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’