Yanga yapigia hesabu mashindano ya CAF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 May 2020
Yanga yapigia hesabu mashindano ya CAF

Uongozi wa klabu ya Yanga umejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri mechi zilizobaki pale ligi itakaporejea huku wakipiga hesabu kali michuano ya kombe la FA ambayo miamba hao wa soka nchini walitinga hatua ya robo fainali

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wamepokea kwa furaha tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kuwa anaweza kuruhusu mashindano mbalimbali ya soka nchini yakaendelea baada ya kujiridhisha hali ya maambukizi ya ugonjwa wa corona

Amesema Yanga inasubiri tamko la TFF kufahamu ni lini michuano hiyo itarejea lakini wao wamejipanga kufanya vizuri kwani hata wakati huu ambao ligi imesimama, nyota wao wanafanya mazoezi kikamilifu

"Tumelipokea kwa furaha tamko la Rais, sasa tunajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye ligi na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ili kupata nafasi ya uwakilishi wa kimataifa mwakani"

"Tunawasubiri TFF waseme lini tunaanza ili tujipange rasmi ila wachezaji wetu wanaendelea na mazoezi kama walivyoelekezwa," amesema Mwakalebela

Kimahesabu Yanga ina nafasi finyu ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu wakiwa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakikusanya alama 51 ambazo ni alama 20 pungufu ya vinara wa ligi hiyo Simba

Hata hivyo Yanga wanaweza kujihakikisha tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho msimu ujao kama wataweza kutwaa taji la FA (ASFC) wakiwa wametinga hatua ya robo fainali

Droo ya hatua hiyo itafanyika Serikali itakaporuhusu kurejea kwa ligi na mashindano mengine

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’