Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli amesema siku za mbele ataruhusu ligi ziendelee nchini hata ikiwezekana bila ya mashabiki ili kuwapa fursa wanamichezo kuendelea kutimiza majukumu yao
Akizungumza mapema leo Mjini Chato katika hafla ya kumuapisha Waziri wa Katiba na Sheria Dk Mwigulu Nchemba ambaye aliteuliwa jana kuchukua nafasi ya marehemu Dk Augustine Mahiga,Β Rais Magufuli amesema takwimu za maambukizi ya corona zinaonyesha kwa wanamichezo na watu wanaofanya mazoezi mara kwa mara hawapati maradhi hayo kwa urahisi
"Siku zinazokuja mbeleni, ninafikiria kuruhusu hata ligi iendelee ili watu wawe wanacheza na wanaangalia kwenye TV na kadhalika, tutaweka utaratibu mzuri tu baada ya kushauriana na wataalamu wetu"
"Ninaelewa, walioathiriwa na corona sijaona mwanamichezo yeyote aliyeathirika sana kwenye hili. Na hii inadhihirisha wazi kwamba kwa wale wanaofanya mazoezi corona inawakwepa"
"Sasa kama tunawazuia wasicheze mpira ina maana tunawaambia waugue corona," amesema Rais Magufuli
Kauli hiyo ya Mh Rais ni wazi itakuwa imekata mzizi wa fitina kuhusu hatma ya ligi kwani amebainisha kuwa ataruhusu iendelee
Β