Mkwasa awapa neno wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Apr 2020
Mkwasa awapa neno wachezaji Yanga

Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa, amesema wachezaji wa klabu hiyo wanapaswa kuendelea na mazoezi binafsi bila kuchoka, wakati wakisubiri hali ya janga la corona kumalizika na kocha wao mkuu, Luc Eymael, kurejea nchini kutoka Ubelgiji.

Eymael amekwama kwao kutokana na janga la virusi vya corona lililosababisha safari za ndege za kimataifa kuzuiwa hadi hali itakapokuwa nzuri.

Mkwasa aliyekuwa ocha wa muda wa Yanga baada ya Mwinyi Zahera kutimuliwa, amewataka wachezaji kuepuka kupata virusi vya corona, lakini pia kutosahau programu walizopewa kila mmoja kwa kujiimarisha kwa mazoezi.

"Wachezaji waendelee na mazoezi huku wakijilinda na virusi vya corona, naamini muda sio mrefu kocha atarejea na kutoa maelekezo mengine, wasichoke wapambane kujenga mwili kimazoezi, "alisema Mkwasa.

Baadhi ya wachezaji wa Yanga wameonekana kuitikia wito wa kufanya mazoezi wakiwa nyumbani kwa muda mrefu sasa.

Hadi ligi inasimama, Yanga ilikuwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 51, nyuma ya Azam inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 54 na vinara Simba wakiongoza kileleni kwa pointi 71.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’