Kabla ya mchezo dhidi ya Stand United, kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina alipata msiba kwao nchini Zambia kwa kufiwa na mtoto wa dada yake.
Hata hivyo alishindwa kuhudhuria msiba huo ili ahakikishe timu yake inafanya vizuri kwenye michezo dhidi ya Simba na Singida United.
Lwandamina amekwenda Zambia kuhani msiba huo katika kipindi hichi cha wiki mbili za kalenda ya FIFA.
Habari za uhakika ni kwamba Lwandamina ameuachia maagizo uongozi wa Yanga uhakikishe unatumia vyema dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Novemba 15 kuweza kusajili wachezaji mahiri kuimarisha kikosi chake.
Mzambia huyo anahitaji kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji sambamba na kujaza nafasi moja ya mchezaji wa Kimataifa.
Kuna tetesi kwamba uongozi wa Yanga umewasiliana na mlinzi wake wa zamani Vicent Bossue kuangalia uwepo wake kabla ya kufanya maamuzi.
Yanga huenda ikasajili wachezaji watatu hadi wanne wakati huu wa dirisha dogo la usajili.

ADVERTISE HERE