Chirwa anasubiri simu tu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Apr 2020
Chirwa anasubiri simu tu Yanga

Nyota wa zamani wa Yanga Obrey Chirwa mkataba wake na Azam Fc unaelekea ukingoni na kuna taarifa za chinichini kuwa mwamba huyo kutoka Zambia ameomba kurejea Yanga

Inaelezwa huko Azam amegomea mazungumzo ya mkataba mpya akitaka jambo hilo lifanyike mwishoni mwa msimu

Chirwa alisajiliwa Yanga mwaka 2015 wakati huo mabingwa hao wa kihistoria wakinolewa na kocha Hans van Pluijm

Inaelezwa ndiye mchezaji ghali zaidi kununuliwa Tanzania kutoka nje ya nchi katika miaka ya karibuni ambapo wakati huo Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji alitoa zaidi ya dola laki mbili kumsajili

Hakuwa na mwanzo mzuri, lakini baadae alikuwa mshambuliaji tegemeo kwenye kikosi cha Yanga

Hata hivyo Chirwa hakuwa mchezaji mvumilivu kwani aligoma kucheza au kusafiri na timu pale alipocheleweshewa mshahara

Miaka mitatu iliyopita ilikuwa migumu sana kwa Yanga kutokana na changamoto za kiuchumi

Mwaka 2018 Chirwa aligoma kuongeza mkataba wake na kuamua kutimkia nchini Misri na kujiunga na timu ya daraja la kwanza

Hata hivyo huko mambo hayakumuendelea vizuri, akarejea dirisha dogo mwishoni mwa mwaka 2018 na akaomba kurudi Yanga

Mwinyi Zahera aliyekuwa kocha wa Yanga akaweka ngumu kumpokea licha ya kumalizana na mabosi wa Yanga akihofia asingedumu kwa kuwa Yanga ilikuwa bado haiko sawa kiuchumi

Zahera akamgomea tena usajili wa dirisha kubwa uliopita akitoa sababu zilezile kuwa Yanga itakapokuwa na changamoto ya fedha atawasumbua

Lakini kwa sasa baada ya GSM kuchukua majukumu ya kugharamia mahitaji ya timu ikiwemo usajili na kulipa mishahara ya wachezaji, pengine unaweza kuwa muda sahihi kwa Chirwa kurejea tena Jangwani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’