Eymael atumia mapumziko ya corona kujiongezea ujuzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2020
Eymael atumia mapumziko ya corona kujiongezea ujuzi

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema wakati huu ambao ligi zimesimama huku akishindwa kusafiri kurejea nchini kutokana na changamoto ya corona, amekuwa akijiongezea ujuzi kupitia utaalamu wa makocha mbalimbali duniani

Eymael amekwama Ubelgiji baada ya kukosa usafiri wa ndege kurejea nchini, Ubelgiji na Tanzania zote zikiwa zimezuia safari za Kimataifa

"Wakati nasubiri ndege ziruhusiwe kutua Tanzania, nimenunua vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na makocha tofauti waliofanikiwa ili kujifunza mbinu mpya na nitakaporudi nitazitumia kwenye michezo iliyosalia pamoja na kuimarisha kikosi kwa msimu unaokuja wa Ligi Kuu Tanzania Bara," amesema

Mbelgiji huyo amesema muda sio mrefu anaweza kurejea nchini, hivyo anatumia kipindi hiki kujiandaa kwa mbinu mpya zitakazomsaidia kutengeneza kikosi chenye ushindani kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa katika msimu unaokuja wa ligi.

Amesema nyumbani muda wote bila kazi inaumiza, lakini kupitia kusoma vitabu itamsaidia kujua mbinu ambazo anaweza akawapa wachezaji wake kulingana na miundo mbinu ya viwanja vilivyopo nchini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’