Msimu uliopita kiungo Ibrahim Ajib alitengeneza historia ya pekee kunako klabu ya Yanga. Alifunga mabao saba na kutoa pasi 17 za mabao, kiufupi ulikuwa msimu mzuri sana kwake
Hata hivyo baada ya mkataba wake kumalizika, aligoma kuongeza mwingine na kutimkia klabu yake ya zamani ya Simba
Huko mambo yamekuwa tofauti kwani mpaka sasa msimu huu ukielekea ukingoni, amefunga bao moja tu na kutoa pasi mbili za mabao
Amekuwa na nafasi finyu kwenye kikosi cha kwanza
Mitandaoni kumekuwa na mjadala ambapo swali linaloulizwa ni kuwa Je iwapo Ibrahim Ajib atarejea Yanga leo, atakuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza?
Jambo moja kubwa ni kuwa Yanga ilimpa heshima kubwa sana Ajib na pengine ndio maana aliweza kupata mafanikio makubwa
Hatusemi huko aliko hapewi heshima lakini ni wazi kipaji alichonacho hakithaminiwi kama alivyokuwa Yanga
Kwani kwa muda mfupi tu, Ajib anaonekana kuwa mchezaji wa kawaida kabisa