Mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo ameshindwa kurejea nchini kutokana na janga la corona
Shikhalo aliruhusiwa kwenda kwao Kenya kushiriki mazishi ya kaka yake aliyefariki dunia hivi karibuni
Hata hivyo kutokana na ugonjwa wa corona kuenea kwa kasi nchini Kenya, Serikali ya nchi hiyo imechukua hatua ya kufunga mipaka ya nchi pamoja na kuzuia wananchi wake kutoka nje
Shikhalo amesema kwa sasa amekuwa na wakati mgumu kufanya mazoezi kutokana na masharti yaliyowekwa nchini humo
"Nalazimika kufanya mazoezi nikiwa ndani tu nikisubiri mambo yatulie niweze kurejea Tanzania kuendelea na majukumu yangu," amesema
Changamoto kama hiyo imemkuta kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael ambaye naye amekwama nchini Ubelgiji
ADVERTISE HERE