Wizara ya Afya imetoa taarifa ya vifo vya wagonjwa wawili waliokuwa wameambukizwa virusi vya corona
Aidha kesi nyingine tano za maambukizi zimeripotiwa jijini Dar es salaam na kesi mbili kuripotiwa visiwani Zanzibar
Idadi ya wagonjwa walioambukizwa wamefikia 32, wagonjwa watano wamepona na wagonjwa 24 wanaendelea na matibabu wakati waliofariki sasa wamefikia watatu
Serikali imewasisitizia wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo kwa kufuata maelekezo yanayotolewa kupitia njia mbalimbali
ADVERTISE HERE