Nina deni kubwa Yanga - Mahadhi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2020
Nina deni kubwa Yanga - Mahadhi

Mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi ambaye amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha, amesema ana deni kubwa na klabu hiyo ambayo ilimnasa kutoka Coastal Union miaka minne iliyopita

Mahadhi anayesubiri kurejea dimbani baada ya janga la corona, ameahidi kupamban kuhakikisha anawapa furaha mashabiki wa Yanga ambao walitarajia kumuona akiisaidia timu kwenye mashindano mbalimbali.

Nyota huyo alisema anaahidi kuendeleza ushindani katika kikosi hicho na kuisaidia Yanga kutimiza malengo yake ya msimu ujao.

"Nina deni kubwa kwa mashabiki wangu pindi Ligi Kuu itakaporejea, nitalipa deni hilo kwa kuendeleza kasi niliyokuwa nayo," alisema Mahadhi.

Alieleza kwa sasa ameshaanza kufanya mazoezi magumu kwa kufuata programu maalumu aliyopewa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm.

"Nafanya mazoezi magumu kuuweka sawa mwili wangu ili kujiandaa na ligi, ninaamini Mungu atanisimamia na kurejea katika kiwango changu," Mahadhi alisema.

Aliendelea kuishukuru Yanga kwa kumpa huduma zote muhimu tangu alipoanza kuumwa na madaktari wanaofuatilia afya yake kwa karibu.

"Ninashukuru ninapata ushirikiano mkubwa kutoka katika klabu yangu, mpaka hapa nilipo sasa siwezi kuisema vibaya timu yangu, wanasimamia huduma zote ninazotakiwa kupata za hospitali," Alisema Mahadhi.

Mahadhi alipata janga la kuvunjika mguu kwenye mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya USM Alger August 2018

Nyota huyo alifanyiwa upasuaji wa goti hilo mara mbili kabla ya Yanga kumpeleka nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’