Afisa Mhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema kama sio janga la Corona, mchakato wa mabadiliko wa klabu hiyo ungekuwa umetangazwa
Nugaz amefichua kuwa walikuwa tayari kuanza kampeni ya elimu na mafunzo kwa Wanachama na Mashabiki wao ili wawe tayari kupokea mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo
Uongozi wa Yanga umesema mchakato huo unatarajiwa kuwekwa hadharani mwezi ujao
"Kila kitu kiko sawa, nawaambia wanachama na mashabiki wetu wakae tayari kupokea mabadiliko, mwezi ujao kila kitu kitakuwa hadharani"
"Tulikuwa tumejipanga kuanza kampeni na kutoa elimu mapema zaidi lakini changamoto ya corona inayotikisa dunia sasa, ikapelekea tusitishe mpango huo," amesema
Aidha Nugaz amesema gharama zote za mchakato huo zitasimamiwa na GSM ambao jana walitangaza kurejea rasmi baada ya mtafaruko uliotokea wiki chache zilizopita baina yao na uongozi wa Yanga kumalizika
Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisin Hersi Said alisema watausimamia na kuhakikisha mchakato huo unakamilika haraka ili kuifanya Yanga ielekee kwenye mfumo wa uendeshaji wa kisasa ambao utavutia wafanyabiashara na wawekezaji wengi kuweka fedha zao