Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Amissi Tambwe alikuwa nchini kwa takribani wiki mbili ambapo pamoja na mambo mengine, alipata nafasi kufanya mazungumzo na Kamati ya Mashindano ya mabingwa hao wa kihistoria
Tambwe aliushuhudia mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba uliopigwa March 08 ambao Mghana Bernard Morrison alipeleka kilio Msimbazi kwa kufunga bao pekee la ushindi
Mbabe huyo wa mipra ya vichwa amesema moja ya masuala waliyojadiri na mabosi wa Yanga ni kuangalia uwezekano wa kumrejesha msimu ujao
"Wiki iliyopita nilikuwa hapo Tanzania, nilifanya mazungumzo ya viongozi wa Yanga, ikiwa ni pamoja na kukutana na viongozi wa Kamati ya Mashindano, wameahidi kunipa nafasi nirejee msimu ujao," alisema Tambwe kwa njia ya simu
"Kwa sasa naona timu imeimarika kwa baadhi ya maeneo kuanzia sehemu ya ulinzi na kiungo, isipokuwa bado ipo changamoto kwenye kufunga, nina uhakika nikija hapo kwa kushirikiana na wachezaji waliopo, tutamaliza tatizo la kupachika mabao"
Tambwe amesema anaamini hakuongezewa mkataba Yanga kwa kuwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera hakuwa akimkubali
Lakini anaamini yeye bado alikuwa na uwezo kuliko washambuliaji wote ambao Zahera aliwasajili ambao hata hivyo mikataba yao ilivunjwa
"Zahera hakuwa ananipa nafasi ili kunikatisha tamaa, badala yake aliwapa nafasi wachezaji aliowasajili hata kama walifanya vibaya," alisema
Pamoja na kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara, Tambwe alimaliza msimu akiwa amefunga mabao nane
Kwa sasa Tambwe anafanya mazoezi kwenye klabu ya VitalβO ya Burundi kujiweka sawa kabla ya kurejea nchini akiwa na matumaini ya kujiungana mabingwa hao wa kihistoria kwa mara ya pili
Tambwe ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na Fanja ya Oman