Rekodi zaibeba Yanga mchezo dhidi ya Singida United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Nov 2017
Rekodi zaibeba Yanga mchezo dhidi ya Singida United
Yanga tayari iko mkoani Singida ambako kesho itashuka kwenye dimba la Namfua kuumana na wenyeji wao, Singida United.

Yanga ina rekodi nzuri dhidi ya timu hiyo katika mechi zao za mwisho za misimu mitatu ambayo Singida iliicheza Ligi Kuu mara ya mwisho.

Singida ilishuka daraja mwaka 2002 baada ya kupanda Ligi Kuu (enzi hizo Ligi Daraja la Kwanza) mwaka 1999 ikifahamika kama Mto FC.

Katika mechi nne walizokutana na Singida, Yanga imeshinda tatu dhidi ya moja na katika mechi yao ya mwisho kukipiga Uwanja wa Namfua, Vijana wa Jangwani waliichana Singida kwa mabao 4-1, na hicho ndicho kinachowafanya watabasamu wakiamini kuwa, wikiendi itakuwa nyepesi kwao ugenini.

Katika mechi hizo Yanga ilianza kwa kuitambia Singida mabao 2-0 nyumbani kabla ya kwenda kulala ugenini Namfua kwa bao 1-0 mwaka 2000 ndipo msimu uliofuata walipoiadhibu vibaya Singida nje ndani.

Walianza kwa kuikandamiza mabao 4-1 katika mechi ya kwanza Namfua kabla ya kuibanjua tena 6-1 katika mechi ya marudiano nyumbani msimu wa 2001.

Msimu wa 2002 ambao Singida ilishuka daraja, timu hizo hazikukutana kabisa kwa vile zilipangwa makundi mawili tofauti, Singida ikiwa Kundi C na kuburuza mkia wakati Yanga ilikuwa Kundi B na ilifanikiwa kutwaa taji mbele ya Simba na Prisons katika hatua ya Nane Bora.

Singida kupitia Katibu Mkuu wao, Abdulrahman Sima ametamba kuizima Yanga kwa vile wanataka kuanza vema kwenye uwanja wao wa Namfua.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’