Matawi Yanga yampongeza Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Mar 2020
Matawi Yanga yampongeza Dk Msolla

Viongozi wa Matawi ya klabu ya Yanga wamempongeza Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla kwa kuchukua hatua ya kuwaondoa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliosababisha mtafaruko ambao ulipelekea Wadhamini wa klabu hiyo kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa

Mratibu wa Matawi, Kais Edwin amesema wao walitoa ombi na wanashukuru uongozi umelifanyia kazi haraka iwezekanavyo kwa manufaa ya Klabu ya Yanga.

Amesema Dk Msolla kaonyesha ukomavu katika uongozi kwa kuwachukulia hatua wahusika hao

"Tulisema kwa kumaanisha, ila Dk Msolla kiongozi msikivu, kalifanyia kazi sasa tunamuomba GSM arejeshe moyo wake nyuma na kuendelea kuisapoti Yanga, haya yamepita arejee kama alivyokuwa akifanya"

Juzi na jana Kamati ya Utendaji ya Yanga ilijifungia nje ya ofisi za Klabu hiyo siku mbili mfululizo kujadili sakata hilo na ndipo jana jioni ikatoka na maazimio ya kuwasimamisha wajumbe wawili huku watatu wakitangaza kujiuzulu wenyewe.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’