Ndemla atajwa tena Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Mar 2020
Ndemla atajwa tena Yanga

Kumekuwa na tetesi za kila mara zinazomuhusisha kiungo wa Simba Said Khamis Ndemla kujiunga na klabu ya Yanga

Ni kila dirisha la usajili linapokaribia, ni lazima jina la Ndemla litajwe kutakiwa Jangwani

Kiungo huyo mwenye mashuti makali, anamaliza mkataba wake na Simba mwishoni mwa msimuΒ  lakini kama ilivyo ada, ameanza kuhusishwa na Yanga

Niyonzima ampa ushauri wa bure

Haruna Niyonzima ambaye amerejea Yanga baad ya kuitumikia Simba kwa misimu miwili, ameeleza kumkubali Ndemla kuwa ni mchezaji mwenye kipaji

Hata hivyo amemshauri kuwa kuendelea kubaki Simba bila ya kupata nafasi ya kucheza kutaharibu kipaji chake

"Ndemla ni mchezaji mzuri, unajua Tanzania imejaaliwa wachezaji wenye vipaji vya mpira lakini huwezi kuwa mchezaji mzuri kama haupati nafasi ya kucheza kwenye timu yako lazima kiwango chako kitaporomoka.

"Namshauri atafute changamoto mpya nje ya Simba ili aimarishe kiwango chake kuliko kuendelea kung'ang'ania kwenye timu ambayo hana nafasi ya kucheza," amesema Noyonzima

Hata hivyo ikitokea Yanga imemsajili Ndemla bado atakabiliwa na changamoto ya kupata nafasi mbele ya nahodha Papy Tshishimbi na Feisal Salum

Lakini mambo yanaweza kubadilika hasa ikitokea kama Tshishimbi ataamua kuondoka

Mara nyingi wachezaji wanaotoka Simba kujiunga na Yanga hufanya vizuri lakini mambo huwa tofauti kwa wale wanaotoka Yanga kwenda Simba

Mfano mzuri ni Ibrahim Ajib na Gadiel Michael waliojiunga na Simba mwanzoni mwa msimu walitokea Yanga

Ajib alisajiliwa na Yanga akitokea Simba ambako huko alikuwa akionekana mchezaji wa kawaida

Lakini misimu yake miwili aliyocheza Yanga ilimfanya awe mchezaji mkubwa hadi kutakiwa na klabu ya TP Mazembe

Pengine atakuwa anajutia uamuzi wake wa kurejea Simba kwani huko amekuwa tena mchezaji wa kawaida

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’