Kama Mwanachama na Shabiki NambaMoja wa Yanga nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya GSM kujiweka kando katika jitihada za kuijenga upya Yanga
Kulingana na barua yao, wamesema watabaki na jukumu lao la kimkataba ambalo ni kutengeneza na kusambaza jezi za klabu
Hili ni pigo kwa Wanayanga wote ambao walikuwa wameanza kuuona mwanga baada ya kutembea vichwa chini tangu alipoondoka Yusuph Manji
Hili ni pigo takatifu kwetu sote sisi ambao Yanga inapokuwa haifanyi vizuri tunaumwa
GSM wametutandika kwelikwei sisi wanyonge ambao furaha yetu ni Yanga, kwani tunafahamu, uamuzi wao huo unakwenda kuturudisha nyuma kwa hatua 99 wakati tulikuwa tumesonga mbele kwa hatua 100
Tunachowaomba GSM, wazungumze na viongozi wa Yanga ili kumaliza changamoto iliyopo. uzuri wao na sisi ni wamoja, tunafahamu wao ni Wanayanga wenzetu
Sisi tunasimama pamoja nao, hatutawaunga mkono viongozi wabinafsi wanaoweka maslahi yao mbele