Mwakalebela afunguka ulipofika mchakato wa Mabadiliko

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Mar 2020
Mwakalebela afunguka ulipofika mchakato wa Mabadiliko

Mkutano Mkuu wa wanachama wa klabu ya Yanga unatarajiwa kufanyika mwezi May ikiwa ni hatua muhimu kuelekea mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema michakato mingine ya ndani inaendelea kufanyika ikisimamiwa na Kamati husika

Aidha amesema baada ya siku 30 za zuio la Serikali, wataitisha Mkutano wa Wanachama kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ambayo yataidhina utaratibu mpya wa kusajili wanachama

Awali Yanga iliitisha Mkutano huo Februari 16 lakini haukufanyika kutokana na mkanganyiko wa kisheria kulingana na Katiba ya Yanga

Yanga imedhamiria kubadili mfumo wake wa uwendeshaji wa klabu hadi kufikia mwishoni mwa msimu huu

Hata hivyo imelenga kufuata utaratibu tofauti na ule unaotumiwa na watani zao Simba

Hivi karibuni Yanga walimleta mtaalam kutoka Ureno ambaye hata hivyo mapendekezo yake yalionekana kuwa na gharama kubwa hivyo uongozi wa Yanga pamoja na wadhamini wao GSM kuamua kuachana nayo

Kwa sasa Yanga inashirikiana na klabu moja ya La Liga ambapo mabingwa hao wa kihistoria wanajifunza mfumo wao wa uendeshaji ili kuweza kuutumia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’