Msimu unakwisha kwa majonzi, tujipange kwa msimu ujao

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
16 Mar 2020
Msimu unakwisha kwa majonzi, tujipange kwa msimu ujao

Ni wazi msimu wa Yanga kwa upande wa ligi kuu umeshamalizika kwani hakuna tena nafasi ya kutwaa ubingwa kwa mechi zilizobaki

Umekuwa msimu uliokuwa na changamoto nyingi za ndani ya uwanja, kwani nje ya uwanja baada ya GSM kuingia, angalau mambo ya kifedha yamekaa sawa

Wakati mwingine tunapaswa kukubali hali halisi, mara chache mafanikio huja kwa bahati, lakini mara nyingi yanahitaji maandalizi

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla pamoja na timu yake ya uongozi, kwa kiasi kikubwa wamejitahidi kuiweka timu kwenye mazingira ya ushindani

Ujio wa GSM kama wadhamini ni juhudi zao, tumeona mabadiliko ya kikosi tangu wakati wa Zahera mpaka sasa Luc Eymael

Pengine mambo haya yalichelewa kufanyika kwani yamekuja wakati robo ya msimu ikiwa tayari imekatika

Bado kuna nafasi kwenye michuano ya kombe la FA (ASFC) huku ndiko ambako kipaumbele kinapaswa kuwekwa

Kwani ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao, Yanga inapaswa kutwaa taji la FA

Huku kuna mechi tatu muhimu, hizi ndizo mechi za kufa nazo

Yanga imedhihirisha ikiwa na jambo lake ikitaka liwe, linakuwa

Majuzi tu mkazo mkubwa uliwekwa kwenye mchezo dhidi ya Simba na ushindi ukapatikana

Nguvu hiyo sasa ihamishiwe kwenye FA, ingawa bado upinzani utakuwa mkubwa kwani huko nako wale watakaopangwa kucheza na Yanga pengine wataahidiwa mamilioni kama ulivyokuwa mchezo wa KMC!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’