Makapu amemzidi Yondani hapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Mar 2020
Makapu amemzidi Yondani hapa

Imani ya Kocha Luc Eymael kwa Juma Saidi ‘Makapu’ ni kubwa kutokana na uwezo wake wa kucheza mipira ya juu kama alivyofanya kwenye mechi dhidi ya Simba. Makapu ana uwezo wa kucheza kwa ufasaha nafasi ya kiungo mkabaji, beki ya kati na kulia.

"Kila mchezaji naamini ana uwezo wake binafsi, sio kwamba Yondani mchezaji mbaya, lakini katika mchezo dhidi ya Simba tuliwafuatilia kwa muda mrefu na kugundua safu yao ya ushambuliaji ina watu warefu.

"Kuna Meddie Kagere na John Bocco wote vimo vyao vimemzidi Yondani lakini Makapu ni mrefu na alifanikiwa kuokoa hatari nyingi zilizokuwa zinaelekea kwetu, kweli Makapu alistahili nafasi hiyo japo wengi walizoea kumwona akicheza nafasi nyingine,” alifafanua Eymael. Makapu alitua kwenye kikosi hicho kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Shangani ya Zanzibar baada ya Yanga kumwona akiichezea Taifa Stars.

Kocha Eymael ametoboa siri ya kumwamini na kumpa nafasi ya kucheza kila wakati, Makapu katika michezo ya hivi karibuni ndani ya chama lake.

Katika mchezo dhidi ya Simba Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Bernad Morrison, kocha huyo alimpanga mchezaji huyo na kumweka nje mkongwe, Yondani ambaye amejijengia ufalme kwa muda mrefu.

Kuhusu kumbadili namba Makapu, kocha huyo alisema hiyo ni mbinu ambayo huitumia kila wakati na humsaidia kuujua uwezo wa wachezaji zaidi ya namba anayocheza.

"Ona sasa wachezaji wengi wameitwa timu ya taifa ina maana kama ulikuwa huna tabia ya kubadilisha na kuwajenga wachezaji kucheza nafasi kadhaa hapa lazima utafeli hesabu zako."

Wachezaji wa Yanga walioitwa kwenye timu ya taifa ni Metacha Mnata, Juma Abdul, Makapu, Mapinduzi Balama Feisal Salum ‘Fei Toto’ Ditram Nchimbi ambao wote walianza katika kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Simba. Pia, Yondani naye ameitwa kwenye kikosi hicho licha ya kucheza dakika tano dhidi ya Simba.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’