Eymael atazifikia alama 86 za Zahera?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Mar 2020
Eymael atazifikia alama 86 za Zahera?

Msimu uliopita pamoja na Yanga kuwa changamoto nyingi, aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera aliwawezesha mabingwa hao wa kihistoria kumaliza ligi wakiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya alama 86

Mpaka wakati huu wa msimu, Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa imekusanya alama 50 baada ya kushuka dimbani mara 26

Kimahesabu, kocha Luc Eymael anaweza kufikisha alama 86 kama vijana wake watashinda mechi zote 12 zilizobaki

Lakini kutokana na ushindani wa ligi ulivyo, pamoja na mwenendo wa kikosi chake, sio jambo jepesi kwa Yanga kuweza kushinda mechi zote 12 zilizobaki

Eymael ameiongoza Yanga katika takribani mechi 15,  ameshinda mechi 8, akipoteza mechi tatu na sare nne

Msimu mzima uliopita Yanga ilipoteza mechi sita na sare tano wakati msimu huu mabingwa hao wa kihistoria mpaka sasa wamepoteza mechi 4 na sare 8

Hata hivyo Eymael takwimu zake zinaweza kupata utetezi kwani alikabidhiwa timu robo ya msimu ikiwa tayari imemalizika

Mabadiliko ya benchi la ufundi pamoja na wachezaji yanaweza kuwa yamechangia kikosi chake kuchelewa kupata muunganiko

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’