Namungo vs Yanga mechi ya kibabe uwanja wa Majaliwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2020
Namungo vs Yanga mechi ya kibabe uwanja wa Majaliwa

Kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kuwasili mkoani Lindi leo tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa uwanja wa Majaliwa, wilaya ya Ruangwa siku ya Jumapili March 15

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara, unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na ubora wa timu zote

Namungo Fc inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama 49, alama moja pungufu ya Yanga yenye alama 50 ikiwa nafasi ya tatu

Hata hivyo Namungo imecheza mchezo mmoja zaidi ya Yanga

Timu hiyo bado haijapoteza mchezo kwenye uwanja wake wa nyumbani msimu huu na watakutana Yanga ambayo imetoka kupoteza mchezo dhidi ya KMC jana

Hii itakuwa mara ya tatu kwa Yanga kucheza kwenye uwanja wa Majaliwa tangu uwanja huo uzinduliwe mwaka jana

Mchezo wa kwanza ulikuwa kwenye hafla ya uzinduzi ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1

Kisha Yanga ikarejea dimbani hapo kwenye mchezo wa kombe la FA na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0

Msimu huu huo ni mchezo wa kwanza kuzikutanisha timu hizo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’