Eymael aanza hesabu za msimu ujao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2020
Eymael aanza hesabu za msimu ujao

Ukweli ni kwamba msimu huu unaelekea ukingoni na Yanga haiwezi kufikia malengo yake ya kutwaa ubingwa ambayo yaliwekwa mwanzoni mwa msimu

Mabadiliko ya kikosi na benchi la ufundi, inaweza kuwa sababu ya kuifanya Yanga isiwe na mwendelezo mzuri

Tangu mwezi Juni mwaka jana, Yanga imesajili wachezaji 22 na kubadilisha benchi la ufundi mara tatu

Sasa ili kuhakikisha msimu ujao timu inakuwa imara, uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wadhamini wao GSM, wamempa kocha Luc Eymael ruhusa ya kuanza kusaka wachezaji anaotaka wasajiliwe

Kocha huyo ametakiwa kuangalia maeneo yenye mapungufu na sio kusajili timu nzima na bila mpango kama ilivyokuwa kwa Mwinyi Zahera

Moja ya maeneo ambayo wanayanga watarajie kuona mabadiliko ni safu ya ushambuliaji

Washambuliaji David Molinga na Yikpe Gnamien wana uwezekano mdogo wa kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao

Molinga alisajiliwa kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Renaissance, anatarajiwa kurejea kwenye klabu hiyo inayoshika nafasi ya tano Ligi Kuu ya DRC

Kwa Gnamien mabosi wa Yanga watalazimika kuvunja mkataba wake kwani alisaini miaka miwili

Eymael ameahidi kuwa ataleta washambuliaji ambao wataifanya safu ya ushambuliaji iwe moto wa kuotea mbali msimu ujao

Amesema anawafahamu wachezaji wazuri ambao watain'garisha safu hiyo kwa kushirikiana na Bernard Morrison na washambuliaji wazawa

Usajili wa Morrison ni pendekezo la Eymael Yanga ikimnasa Januari 15, siku ambayo dirisha dogo la usajili lilifungwa

Habari njema ni kuwa Yanga inakaribia kubadili mfumo wake wa uendeshaji na pengine msimu ujao itakuwa mikononi mwa wawekezaji hivyo suala la kusajili wachezaji wakali halitakuwa tatizo kwani fedha itakuwepo

Kuna uwezekano mkubwa GSM wakajitosa 'mazima' kuwekeza Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’