Morrison apagawa na wazimu wa mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Mar 2020
Morrison apagawa na wazimu wa mashabiki Yanga

Mshambuliaji wa Yanga Bernad Morrison amesema uwepo wa mashabiki wengi wa Yanga, katika mchezo wao dhidi ya Simba, ulimpa morali kubwa kiasi cha kuhisi anaweza kufanya kila kitu uwanjani.

Morrison amesema ushindi waliopata mbele ya Simba ulichagizwa pakubwa na shangwe na kelele zilizopigwa na mashabiki wa Yanga katika dakika zote 90, huku akifunguka kuwa hakutarajia kama mashabiki hao wangekuwa ‘vichaa’ wa soka.

Morrison ndiye aliyeipa ushindi Yanga wa bao 1-0, mbele ya Simba katika mchezo uliochezwa Machi 8, katika Uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Ahmad Ahmad.

"Mashabiki wa Yanga walikuwa katika ubora wao, walipiga kelele ambazo mimi binafsi ziliniongezea morali na kuona kuwa naweza nikafanya kila kitu nikiwa na mpira"

"Kiukweli niwashukuru sana, maana kila mchezaji wa Yanga alionekana kuwa na nguvu sana, ushindi tuliopata ulisababishwa na nguvu yao.

"Niwaombe wasiache kufanya hivyo, ilinishangaza sana, ukishika mpira wanashangilia, ukiwa unashambulia wanashangilia, ilinipa maswali sana kuwa walikuwa wanahitaji nini, nikagundua kuwa wanahitaji bao na kwa bahati nzuri nilifanya hivyo, lakini kiukweli walinipa hamasa kubwa sana, ninawashukuru sana," alisema Morrison.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’