Yanga yafunguka mgao wa Milioni 200

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Mar 2020
Yanga yafunguka mgao wa Milioni 200

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wachezaji watapata mgao wao wa Tsh Milioni 200 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa Jumapili iliyopita

Bumbuli amesema fedha hizo zitagawiwa kulingana na ushiriki wa kila mchezaji katika mchezo huo

"Kwanza tuna wale wachezaji 14 ambao walikuwa dimbani siku ya mchezo, wao watakuwa na mgao wao"

"Pili wale wengine ambao walikuwemo kwenye kikosi cha wachezaji 18 wa mchezo lakini hawakupata nafasi ya kucheza watakuwa na mgao wao"

"Lakini wapo wachezaji ambao ni miongoni mwa wale 23 ambao waliingia kambini kujiandaa na mchezo, wao pia watakuwa na mgao wao"

"Mwisho kabisa ni wachezaji wengine ambao ni miongoni mwa wachezaji 29 tuliowasajili nao watapata mgao"

"Hatutawasahau viongozi wetu wa benchi la ufundi pia watakuwa na mgao wao"

"Fedha tayari zipo kinachosubiriwa ni kukamilika kwa michakato ya ndani ili wahusika wapate haki yao," amesema Bumbuli

Wadhamini wa Yanga kampuni ya GSM iliahidi kutoa kitita hicho kama Yanga ingeibuka na ushindi dhidi ya Simba, matokeo ambayo yalipatikana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’