Ushindi una raha yake bhana! Hali ndivyo ilivyo mtaani baada ya ushindi wa jana waliopata Yanga kwa kuifunga Simba bao 1-0
Ukweli ni kwamba kabla ya mchezo huo mashabiki wa Simba walitamba kila kona wakiamini kuwa timu yao ingeshinda mabao mengi
Wapo waliotishia kuwa wangetembea uchi kama Yanga ingeifunga Simba jana
Hata msemaji wa Simba Haji Manara aliahidi kuwa angetembea kwa mguu kutoka barani Ulaya mpaka Afrika kama Yanga ingeshinda
Pamoja na mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa jana, muda pekee walioishangilia timu yao, pengine ni wakati timu zikiingia uwanjani
Ni kwa sababu Yanga walikuwa bora na hatari pale walipokuwa na mpira
Ni ushindi wa heshima kwa Yanga kwani walizima kelele za mashabiki kutoka kila upande wa Tanzania
Ni haki kwa mashabiki wa Yanga kufurahia ushindi huu kwani wale wa upande wa pili walidhani wamepewa haki miliki ya ushindi katika michezo ya dabi