Uzoefu wa 'dabi' kumbeba Eymael mechi dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Mar 2020
Uzoefu wa 'dabi' kumbeba Eymael mechi dhidi ya Simba

Keshokutwa Jumapili March 08, kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael anakabiliwa na mtihani wake wa kwanza wa mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Taifa

Eymael alijiunga na Yanga mwezi Januari 2020 siku chache baada ya kupigwa mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2

Wakati Yanga ikicheza mechi ya kwanza ilikuwa ikisimamiwa na kocha Charles Mkwasa ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa mabingwa hao wa kihistoria

Inafahamika michezo ya dabi huongoza kuwaweka makocha na wachezaji matatani lakini Eymael amesema anakwenda kuikabili Simba bila presha yoyote

Mbelgiji huyo aliyefanya kazi mataifa mbalimbali barani Afrika, ametamba kuwa na uzoefu wa michezo ya aina hiyo

Pamoja na kufanya kazi kwa muda mrefu ligi kuu ya Afrika Kusini, Eymael amewahi kuionoa klabu ya AS Vita inayoshiriki ligi kuu ya DR Congo

Wakati yuko Congo mchezo wake mkubwa wa dabi ulikuwa dhidi ya TP Mazembe

Lakini pia amewahi kuinoa AFC Leopards ya Kenya ambayo ina upinzani mkali na klabu ya Gor Mahia mchezo baina ya timu hizo ukipachikwa jina la 'mashemeji dabi'. Huu ndio mchezo mkubwa zaidi kwa ligi ku ya Kenya

Akiwa Sudan aliinoa klabu ya Al Hilal ambayo ina upinzani mkubwa na klabu ya El Marrikh, mchezo baina ya timu hizo ukiwa ndio mchezo mkubwa zaidi nchini Sudan

Eymael amesema kuelekea mchezo huo haangalii matokeo ambayo wapinzani wake wamepata michezo ya nyuma, anaiandaa timu yake kimbinu ili kuweza kuibuka na ushindi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’