Ujio wa Rais CAF kuongeza umakini mpambano wa watani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Mar 2020
Ujio wa Rais CAF kuongeza umakini mpambano wa watani

Ujio wa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad, umebadilisha utaratibu wa mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, tofauti na ilivyozoeleka ili kuipa hadhi ya kimataifa.

Mchezo huo wa pili wa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unazikutanisha timu hizo kongwe, ikiwa ni baada ya kutoka sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Yusuf Singo, alisema siku ya mchezo huo kutakuwa na mabadiliko katika maeneo mbalimbali hadi jinsi ya kuingia uwanjani.

Singo alisema wamefanya hivyo ili kuimarisha usalama, pamoja na kulipa hadhi pambano hilo kutokana na ugeni unaoongozwa na Rais wa CAF.

Alisema kutakuwa na utaratibi mpya wa eneo la VVIP kiasi kwamba hakuna mtu atakayeruhusiwa kukaa sehemu bila kuwa na kadi maalum ya mwaliko.

Singo alisema kumekuwa na mazoea ya kukaa eneo hilo hata watu wasiohusika na kulifanya lishuke hadhi yake kwa sababu watu wanajaa zaidi ya idadi inayotakiwa.

“Watu wamekuwa wakijazana sana VVIP, tunapunguza msongamano huo kuanzia mechi ya Yanga na Simba, kutakuwa na kadi za mwaliko, kama mtu hajapata, asijaribu kulisogelea, atafute utaratibu mwingine.

“Kadi zinazotolewa zitakuwa na jina la mtu husika na endapo hatakuja kwenye mechi na kumpa mtu mwingine, hataruhusiwa, kadi ni ya mtu mmoja hakuna kuongeza.

“Lile eneo lina hadhi yake na idadi ya watu wanaotakiwa kukaa, lakini kwa sasa linaonekana kuzoeleka, inafika kipindi watu wengi hadi kukosa viti na hata sambusa zinazoandaliwa, tunagombea,” alisema Singo.

Alieleza kuwa ukaguzi wa watu wanaokwenda kukaa eneo hilo utaanizia chini, tofauti na awali na magari yataingia yenye kadi.

Singo alifafanua kuwa barabarainayotokea Chuo cha Duse, itafungwa na magari yametengewa eneo maalum la kupaki ambalo ni ofisi za zamani za Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Naye Ofisa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (C.E.O), Almasi Kasongo, alisema wamejipanga vizuri kila eneo na anatarajia kuona Watanzania wanadumisha utamaduni wa kujaza uwanja.

Alisema anataka kuona watu wengi kwa sababu Ahmad Ahmad ameomba kuja Tanzania baada ya kuvutiwa na mashabiki wa Yanga na Simba wanavyojaza uwanja.

“Rais wa CAF amekuja katika mchezo kutokana na matukio aliyoshudia katika  mchezo uliopita wa utani, hamasa na tamaduni za watani wa jadi na kuomba kuja kuona mechi hiyo,” alisema Kasongo.

Alisema kikao cha mechi kitafanyika siku moja kabla na si siku ya mchezo kama ilivyozoeleka, lakini vikosi vitawasilishwa kwa utaratibu wa kawaida

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’