Bao langu ni zawadi kwa mashabiki wa Yanga - Chirwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Oct 2017
Bao langu ni zawadi kwa mashabiki wa Yanga - Chirwa
Kitendo cha kuifungia timu yake bao la kusawazisha jana katika mchezo dhidi ya Simba kumetimiza malengo ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa, ambaye tangu atue kwenye timu hiyo hakuwahi kuwafunga Simba.

Chirwa amesema bao la jana amelitoa zawadi kwa mashabiki wa timu hiyo ambao walifika kwa wingi kuwashangilia na kufanikiwa kusawazisha bao hilo baada ya Shiza Kichuya kutangulia kuwafunga.

"Kilicho nifurahisha ni bao ambalo nimeifunga Simba, kwasababu ndoto zangu siku zote tangu nije Tanzania ni kuifunga timu yenye upinzani na Yanga na siyo niyingine bali ni Simba, na kwakulifanikisha hilo nimeamua kutoa bao hilo kama zawadi kwa mashabiki wote wa Yanga," amesema Chirwa.

Mzambia huyo aliyefikisha mabao matatu hivisasa, amesema baada ya sare hiyo anaamini bado moto wa mabao ataendelea kuuwasha yeye na mshambuliaji mwenzake Ibrahim Ajibu ambaye kwasasa ndiyo kinara wa mabao kwenye klabu hiyo akiwa na mabao 5.

Mshambuliaji huyo ametamba kuwa malengo yake msimu huu, ni kuhakikisha anavuka kiwango cha mabao 12, aliyofunga msimu uliopita na ikiwezekana aweze kuibuka mfungaji bora na kutwaa tuzo ya mfungaji bora kwa mara yake ya kwanza.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’