Pasi 27 walipigiwa Alliance Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Mar 2020
Pasi 27 walipigiwa Alliance Fc

Jambo moja la uhakika ambalo kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael amefanikiwa, ni kuwafanya wachezaji wake wafurahie kucheza 'sexy-football' maarufu kama tiki-taka

Yaani ukiwaangalia Yanga walivyocheza dhidi ya Alliance Fc jana, kama wangetumia zile jezi zao zenye rangi ya manjano ungeweza kudhani ni FC Barcelona wakiwa kwenye jezi yao ya ugenini!

Katika michezo ambayo Yanga ilitawala, basi huu dhidi ya Alliance Fc ilifunika!

Kuna wakati Yanga iliweza kupiga mpaka pasi 27 huku wakiongoza umiliki wa mpira kwa asilimia 70 dhidi ya 30 za Alliance

Ndio, changamoto inaweza kuwepo kwenye umaliziaji wa nafasi kwa upande wa washambuliaji lakini ukweli utabaki vilevile kuwa Yanga hii ya Luc ni moto wa kuotea mbali hasa pale wanapoamua kuupiga mpira

Kwanza imebarikiwa wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa wa umiliki wa mpira

Feisal Salum, Haruna Niyonzima, Mapinduzi Balama, Mohammed Issa 'Banka', Bernard Morrison, Mrisho Ngasa, Papy Tshishimbi ni aina ya wachezaji ambao mpira ukikaa mguuni unatulia

Ni kama Wanayanga wamechelewa kuanza kupata burudani kutoka kwa timu yao kutokana na mabadiliko ya hapa na pale yaliyofanyika

Lakini bila shaka kama timu hii itabaki hivi mpaka msimu ujao, na dirisha la usajili nguvu zikaongezwa kwenye maeneo yenye mapungufu hasa safu ya ushambuliaji, nadhani furaha itarejea 'mazima' Jangwani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’