Mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo amewataka mashabiki wa timu hiyo waendelee kuwaunga mkono kwani anaamini upepo wa matokeo mabaya utapita
Kabla ya ushindi wa bao 1-0 juzi dhidi ya Gwambina Fc kwenye mchezo wa kombe la FA, Yanga ilitoka kulazimishwa sare katika michezo minne mfululizo
Shikhalo aliyetua Yanga kutoka Bandari Fc ya Kenya, amesema ni kipindi tu ambacho kinapita
"Mashabiki waendelee kutuunga mkono, wasikatishwe tamaa na matokeo tuliyopata nyuma, ni upepo tu ambao naamini utapita," amesema
Jioni ya leo Jumamosi, saa moja, Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kumenyana na Alliance Fc katika mchezo wa ligi kuu ambao mabingwa hao wa kihistoria watajitaji kuondoka na alama zote tatu
ADVERTISE HERE