Mayay awapa tano Gwambina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Feb 2020
Mayay awapa tano Gwambina

Ally Mayay nyota wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, amesema Gwambina Fc walikuwa bora kwenye mchezo dhidi ya Yanga lakini waliangushwa na kukosa uzoefu

Katika mchezo huo ambao Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0, Mayay ambaye ni Mjumbe wa kamati ya Ufundi, amesema tofauti ya uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kati ya timu hizo ndio ulioipa Yanga ushindi na sio mbinu za kiufundi

"Mechi nyingi kama hizi kati ya timu yenye uzoefu na isiyo na uzoefu, mara nyingi zinaamuliwa na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja"

"Mechi imeamuliwa na uthubutu wa Niyonzima na sio mbinu za kifundi," amesema Mayay

"Gwambina walicheza na kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa ndio maana Yanga waliongoza kwa kufanya faulo nyingi lakini uthubutu wa kujaribu kufunga kwa upande wa Gwambina ulikuwa mdogo ukilinganisha na Yanga. Na hiyo ndio tofauti kubwa kwani kiufundi hakukuwa na tofauti yoyote kiuchezaji," alisema Mayay

Kocha Mkuu wa Yanga LUc Eymael pia aliwasifu vijana hao wanaoshiriki ligi daraja la kwanza kuwa waliwapa wakati mgumu

Gwambina inaongoza kundi B kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza wakiwa wamejikusanyia alama 31 baada ya kushuka dimbani mara 15

Wana nafasi kubwa ya kupanda ligi kuu

Timu hiyo imesheheni wachezaji ambao wana uzoefu wa ligi kuu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’